Domo Kaya

Kimya!
Punguza kelele,
Kasheshe mingi hatuhitaji,
Tumekuskia awali,
Ahadi zako za maziwa na asali,
Ilhali ukishaingia bungeni
Hutujui,hutujali,hututambui,
Kimya mwanangu,
Tumeyaona yote,
Miaka kuja,miaka raudi,
Mabweha kwenye ngozi ya kondoo,
Kazi ni kukula,kujaza vitambi
Na kushughulikia maslahi tu yenu,
Jamii zenu
Na mali yenu.
Sisi vijana bado tuko papa hapa,
Ulipo tuacha miaka nne kale,
Ahadi za kazi,na kazi kwa vijana,
Kuchimba bara bara na kulipwa change
Baada ya hawa mababa kula pesa zote,
Kimya!
Udaku na ulafi wako
Hutakuruhusu kuona masaibu yetu,
Sio maji,sio madawa,sio usalama
Maneno yenyu ya kifedhuli fedhuli
Na uwaminifu sawa na hawa maharamia,
Uraibu wa kitaifa,
Kupasha watoto wetu mimba na ndoto
Za phirauni,
Kimya mwanangu,
Mimi simpumbavu unavyodhania,
Nilikuona jana,nilikuskia juzi
Kabla hujapanga maneno yako ya vurugu,
Kabla hujabebwa na hiyo gari yako ya kifahari
Na kuja kujaza maskio yetu na ujinga wako wa udaku,
Kimya!kimya!kimya!
Hii kelele imezidii,
Tazama mimi maskini wa mali
Tajiri wa akili,
Kimya Mr.Big Man,
Maskio nataftia pamba sasa.
Kesho yaja,silali na haya mateso,
Yatakuwa kwa mawazo,lakini
Yako ni mekulia ndimu,
Kesho ni yangu na wengi sisi ulio waacha taabani.
™©Mwangi Njoroge

Comments

Popular posts from this blog

Book reviews : momo the monkey arrives & momo makes a mess

The 99% Club